FenichaMarket
FenichaMarket

Pakua App Yetu!

Kwa matumizi bora na kufanya maagizo

Kufanya maagizo kwa urahisi
Kupata taarifa za bei na ofa
Kuwasiliana na wauzaji moja kwa moja

Sera ya Kurudisha Bidhaa

Hati ya Kisheria

Sera hii inaelezea mchakato wa kurudisha bidhaa kwenye jukwaa la Fenicha Marketplace.

Muda wa Kurudisha Bidhaa

Wateja wana haki ya kurudisha bidhaa ndani ya siku 7 tangu tarehe ya kupokea bidhaa, ikiwa bidhaa:

  • Ina kasoro ya kiwanda
  • Haikidhi maelezo kama ilivyotangazwa
  • Imeharibika wakati wa usafirishaji
  • Imetolewa kwa makosa (bidhaa tofauti na iliyoagizwa)

Masharti ya Kurudisha Bidhaa

  • Bidhaa lazima iwe katika hali yake ya asili, isiyotumika, na yenye vifungashio vyake vyote
  • Lazima uwasilishe uthibitisho wa ununuzi (ticket/order number)
  • Gharama za kurudisha bidhaa zinalipwa na mnunuzi, isipokuwa kwa bidhaa zenye kasoro

Mchakato wa Kurudisha Bidhaa

  1. Wasiliana na muuzaji kupitia app yetu
  2. Elezea sababu ya kurudisha bidhaa
  3. Muuzaji atakubali au kukataa ombi lako ndani ya siku 2
  4. Ukikubaliwa, rudisha bidhaa kwa anwani itakayotolewa
  5. Baada ya bidhaa kupokelewa na kukaguliwa, utapokea pesa zako ndani ya siku 5-7

Kutolipwa Fedha (Refund)

Mara baada ya bidhaa kukubaliwa kurejeshwa, fedha zitarudishwa kwa njia ile ile uliyolipia (M-Pesa, Airtel, au HaloPesa) ndani ya siku 7 za kazi.

Bidhaa Zisizorudishwa

  • Bidhaa zilizotengenezwa kwa ombi maalum
  • Bidhaa za usafi (mattresses, pillows)
  • Bidhaa zilizotumika au kuharibiwa na mnunuzi

Kwa maswali yoyote kuhusu kurudisha bidhaa
Wasiliana nasi kwa simu: +255 682 484 520 au barua pepe: returns@fenichamarket.co.tz